Burudani

Bob Junior agwaya level za Aslay, atangaza kolabo na Chid Benz

Msanii wa Bongo Flava, Bob Junior ameeleza sababu ya kusitisha kutoa ngoma nyingine kama alivyotangaza hapo awali.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Give Me’ aliwahi kusema baada ya wiki mbili angetoa ngoma nyingine kama anavyofanya msanii Aslay.

Akizungumza na E-Newz ya EATV amesema menejiment yake imeshauri waache kwanza ngoma iendee kisha wiki mbili mbele atakuja na kolabo na Chidi Benz.

“Wahenga wanasema mshika mawali moja humponyoka ili neno lina uzito wake, ni vema ukasikiliza wahenga na muda mwingine ukawa na maamuzi yako,” amesema Bob Junior.

“Tutengemee ni wimbo mimi na Chidi Benz kuliko nyimbo mbili pekee yangu lakini wakaona iwe collaboration wimbo unaitwa Sura Mbili,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents