DStv Inogilee!

Bob Junior amtaja Diamond ndiye analengwa katika madongo yake (+Video)

Msanii  na mtayarishaji wa muziki kutoka studio za Sharobaro rekodi, Bob Junior ameamua kutaja jina la msanii Diamond Platnumz kuwa ndiye anaye lengwa na madongo anayoyatoa kupitia mtandao wa Instagram kwa sasa.

Akiongea na Bongo5, Bob amesemakuwa yeye harushi madongo kama wanavyotafsiri watu bali yeye anachokiongea ni ukweli mtupu kwa msanii huyo.

“Hamna madongo mimi nimeongea fact, nimeongea ukweli na ukweli ubaki kuwa ukweli. Mimi naishi katika ukweli maisha yangu yote nikiamua kumsaidia mtu namsaidia hadi nguvu yangu ya mwisho anasimama, chochote ulichokiona Instagram yangu vingi ni vya ukweli.” amesema msanii huyo.

Pia akaongeza kuwa ” Kuna mtu naye anajiita simba na yeye ndiyo muhusika inamuhusu hiyo. Nimekuwa ni kifanya naye kazi sana lakini dharau na kebehi imetawala sana kwake kuja kwangu, nimefanya naye kazi kwa mapenzi ya mwenyezi mungu kwa sababu wakati anakuja alikuwa akirap nikamshauri aachane na kurap tuimbe.Nikaja nikamfanyia albamu ambayo ilifanya vizuri kutoka kwangu, ‘kamwambie’ bwana Nassibu Diamond Platnumz ni nyimbo ya kwanza kufanya naye na ikampa tuzo tatu, ni nyimbo ambayo mpaka leo hii sikuchukua hata shilingi moja.”

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW