Habari

Bobby Brown hajafurahishwa na kitendo cha binti yake Bobbi Kristina kuchumbiwa

Vaa viatu vya Bobby Brown, pale unapokuja kusikia au kusoma kwenye mtandao binti yako kipenzi amechumbiwa na ‘kaka’ yake tena bila wewe kupewa taarifa, ungechukia right?

Bobby brown

Hivi karibuni mtoto wa kike wa wanamuziki wakongwe marehemu Whitney Houston na mwimbaji wa R & B Bobby Brown alichumbiwa na Nick Gordon, kijana ambaye alilelewa na Whitney Houston kama mtoto wake wa kumzaa na hivyo kuwa kama sehemu ya familia kiasi cha kuwa kama kaka kwa Bobbi Kristina Brown.

Wawili hao wamekumbana na lawama nyingi kutoka kwa watu ambao hawakuzipokea vizuri taarifa hizo kwa madai kuwa kutokana na jinsi ambavyo Nick alipewa malezi na Whitney alistahili kumheshimu Kristina kama dada yake.

Baba wa Kristina ambaye hakuwa ameongea chochote hatimaye amezungumzia swala hilo and guess what? Amemaind sana kwa binti yake kuchumbiwa bila kuombwa “her hand in marriage” na kijana huyo.

Bobbi n nick..

Brown baada ya kuulizwa na TMZ anajisikiaje kuhusiana na binti yake anayetegemea kuolewa, alijibu hajafurahishwa na hilo.

Kinachoonesha kuwa tatizo katika uhusiano wa Bobbi Kristina na mchumba wake Nick Gordon kwa Bobby Brown ni kimoja tu, analalamika kuwa Gordon hakuthubutu hata kumpigia simu kwaajili ya kuomba baraka zake.

Historia ya familia hiyo inaonesha kuwa Bobbi Brown hakuwa na mahusiano mazuri na baba yake kiasi ambacho baada ya kifo cha mama yake (February 11, 2012) alifikiria juu ya kubadili jina lake la mwisho atumie Bobbi Houston kama sehemu ya kumuenzi mama yake pia. Lakini Whitney aliwahi kumsihi asije kufanya hivyo

Hata hivyo pamoja na kwamba Bobbi Kristina haongei na baba yake lakini Bobby Brown amekili kwamba anataka binti yake awe na furaha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents