Habari

Bobby Brown kunyemelea Hela za Whitney Houston

Mume wa Marehemu Whitney Houston, msanii Bobby Brown amekumbwa na tuhuma za kutaka kujipatia mali za ex wife wake ambaye sasa ni marehemu kupitia mtoto wao Bobbi Christina.

Tuhuma hizo zimetolewa na mama wa marehemu Whitney Houston, Cissy Houston, ambaye amemuonya Bobby Brown kwa kutojiweka karibu akidhania atapata japo chochote, na kufikia kumuonya kutoshiriki kwenye mazishi ya msanii huyo.

Mtoto wa Bob na Whitney,Bobbi Christina ndiye mrithi pekee aliyeachwa na Whitney.

Chanzo cha kifo cha msanii Whiutney kimegundulika kua ni matumizi ya madawa ya kulevya yaliyozidia, tabia ambayo wengi wanasema aliitoa kwa Mume wake wa zamani, Bobbi Brown.

Ingawa wengi wamesema Whitney anaweza akawa hajaacha hela zozote, kampuni ya Forbes Marekani, ambayo inafuatilia hela za wasanii wengi wanazoingiza, imesemakwamba Whitney ana mali zinzofikia dola milioni 20.

Wasemaji wa Bobbi Brown wamesema kwamba Bobbi anataka kuwepo kama Baba wa mtoto wake na kumsaidia katika kipindi hiki kigumu alichokua nacho.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents