Habari

Bobi Wine akamatwa na jeshi la polisi Uganda, waandishi wa habari na wananchi warushwa kichura

Msanii wa muziki na Mbunge wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine amekamatwa tena  na jeshi la polisi nchini humo leo mapema baada ya kuwasili Uwanja wa ndege mjini Entebbe akitokea Marekani alikokuwa anatibiwa.

Bobi Wine mwenye kofia nyekundu

Bado hakuna taarifa rasmi ya jeshi la polisi juu ya kukamatwa kwa Bobi Wine, lakini tayari mamia ya watu wakiwemo waandishi wa habari waliojitokeza kumpokea Bobi Wine mjini Entebbe.

Jana jeshi la polisi nchini humo, lilitangaza kuwa hakuna mtu atakayeruhusiwa kumpokea Bobi Wine ndani au nje ya Uwanja wa ndege isipokuwa familia yake tu.

Tayari watu wanne ndugu zake na Bobi Wine wamekamatwa mchana wa leo huku, mamia ya wananchi waliokaidi amri ya jeshi wakivurumushwa na maji ya washa washa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents