Siasa

Bobi Wine ana siku nne za kupinga matokea mahakamani

Kama vikosi vya usalama vitaondoka mara moja nyumbani kwa Bobi Wine, mwanasiasa huyo bado ana siku zipatazo nne kuwasilisha ombi lake mahakamani ili kupinga matokeo.

Kama atafanya hivyo, basi korti itapaswa kusikiliza kesi yake na kutoa uamuzi juu ya ombi lake ndani ya siku 30.

Chama cha National Unity Platform iliiambia BBC kuwa bado walikuwa hawajajipanga kutumia njia hiyo kwa kuwa mgombea wao wa urais alikuwa hawawezi kumpata.

Kupitia matangazo mubashara ya Facebook aliyoyatoa Bobi Wine siku ya Ijumaa, alisema raia wa Uganda wana haki ya kuandamana wanavyotaka, ingawa hakutaka wafuasi wake kuchukua uamuzi huo wa kuingia barabarani kuandamana.

Bobi Wine si kiongozi wa kwanza wa upinzani kufungiwa nyumbani kwake.

Kizza Besigye alifungiwa nyumbani kwake kwa muda wa miezi miwili baada ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2016.

Kufuatia uchaguzi wa mwaka 2011 , Dr Besigye alizindua kampeni ya watu kutembea kuelekea kazini, badala ya kupinga matokeo mahakamani.

Maandamano hayo yalivurugwa na vikosi vya usalama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents