Habari

Bobi Wine apigiwa magoti na polisi wa Uganda

By  | 

Jeshi la polisi nchini Uganda limemuomba Mbunge mpya wa jimbo la Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi Sentamu maarufu kama Bobi Wine kufanya naye kazi ya kuimarisha ulinzi katika eneo hilo.

Bobi ambaye alishinda nafasi hiyo Alhamisi iliyopita, amekuwa akipendwa hasa na vijana wa eneo hilo na ndiyo sababu kubwa ya kuombwa na jeshi hilo kushirikiana katika kulinda eneo lao.

Katika kikao cha polisi kilichofanywa Jumamtatu hii, msemaji wa polisi Asan Kasingye,  amemtaka Mbuge huyo ambaye pia ni msanii wa muziki kusaidia polisi kuweza kupambana na uhalifu kwa kuwa anakundi kubwa la vijana wanaomkubali na kumsikiliza.

“We urge the new MP to work closely with the police within Kyadondo East in order to promote security in the area especially through community policing programmes,” amesema msemaji huyo.

Na Laila Sued

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments