Burudani

Bobi Wine awashukuru Polisi wa Uganda kwa kutoa ulinzi mzuri katika tamasha lake la kwanza tangu akamatwe

Bobi Wine awashukuru Polisi wa Uganda kwa kutoa ulinzi mzuri katika tamasha lake la kwanza tangu akamatwe

Nyota wa muziki wa pop na mbunge wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amefanya tamasha lake kwanza tangu ashtakiwe na kufungwa kwa mshtaka ya uhaini. Kulikuwa na idadi kubwa ya polisi kwenye tamasha hilo, ambalo liliruhusiwa tu kufanyika kwa sababu halikuwa la kisiasa.

Kwa mujibu wa BBC, Bobi Wine anadaiwa kuteswa na kupigwa akiwa kuzuizi mwezi Agosti, madai yanayokanwa na mamlaka. Umaarufu wake miongoni mwa vijana nchini Uganda unaonekana kuwa changamoto kubwa kwa rais wa miaka mingi Yoweri Museveni. Baadhi ya maelfu ya watu waliohudhuria tamasha walivaa nguo nyekundu, rangi inayohusishwa na vuguvugu la Bobi Wine la People Power.

“Ninashukuru polisi wa Uganda kwa kutupa ulinzi na kutotuzuia kama vile wamekuwa wakifanya awali,” Bobi Wine aliuambia umati kwa mujibu wa AFP. “Sisi ni watu wenye amani na tunataka kusikilizwa.”

Mbunge huyo mwenye miaka 36 ambaye jina lake kamili ni Robert Kyagulanyi, aliwania na kushinda kama mgombea huru kwenye uchaguzi mdogo huko Kyadondo East kati kati mwa Uganda.  Mwezi Agosti yeye pamoja na wanasiasa wengine 30 wa upinzani walishtakiwa kwa uhaini baada ya msafara wa rais kutupiwa mawe baada ya mkutano wa kampeni.

Aliondoka nchini Uganda kwenda kupata matibabu nchini Marekani kufuatia majeraha aliyoyapata akiwa kizuizini lakini akarudi nyumbani mwezi Septemba.

Idadi kubwa ya watu nchini Uganda wako chini ya miaka 35 na Wine amekuwa kama mfano wa vijana wenye ghadhabu ya ukosefu wa ajira na siasa zilizokwama.

Bobi Wine alizaliwa miaka minne kabla ya Bw Museveni kuwa rais mwaka 1986 na amekuwa akitoa wito kwa Museveni astaafu kutokana kwa siasa za mwaka 2021.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents