Habari

Bodaboda kuja na muonekano mpya Dar

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amezindua mpango maalumu wa waendesha bodaboda pamoja na bajaji utakaotumika kuwatambulisha sehemu wanazokaa au kupaki.

11

Akizungumza hayo jijini Dar katika viwanja vya Leaders Club, Makonda alisema utaratibu huo ni maalum kwani sheria itatumika endapo watakaokiuka kutovaa makoti maalumu pamoja na namba ambazo wamepewa.

“Suala la helmet halisubiri tarehe moja, ukiwa hujavaa halafu ukapita mahala hapo huna helmet trafki hakusumbui, anakutaka utii makubaliano. Nataka nyie muwe marafiki wa hawa na hawa wawe rafiki zenu, mnafikaje yale yaliyokubaliwa, yaliyokubalika, yaliyo kwenye utaratibu, kila mmoja anatumika kwa upande wake,” alisema.

Aidha Makonda aliwataka waendesha bodaboda kuwa mabalozi wa wenzao wanaovunja sheria za barabara kwa kupakiza abiria zaidi ya mmoja kama (Mshkaki).

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents