Bongo Movie

Bodi ya Filamu kuanzisha Application ili kukuza kazi za Filamu nchini(+Video)

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce G. Fisso amebainisha kuwa bodi hiyo inatarajia kuanzisha Application ili kurahisisha kazi mbalimbali za filamu.


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce G. Fisso

Akiongea na Bongo5 amesema kuwa ukuaji wa teknologia utailazimu bodi hiyo kuendana na hali ya sasa.

“Bodi ya filamu inafikiria kuanzisha Application itakayoweza kurahisisha kazi mbalimbali za filamu vile vile wasanii hawakatazwi kuanzisha Application zao,” amesema Joyce.

Hata hivyo Joyce ameeleza kufurahishwa na mwitikio wa wasanii hao na kuwashukuru vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kufikisha ujumbe kwa wahusika.

“Nina furaha sana kwa sababu tulitarajia wanafilamu na wanatasnia 300 lakini ambo wamefika ni takribani 478, kwa hiyo unaweza kuona jinsi gani ambavyo nina wiwa na kuwashukuru sana wanafilamu kwa kukutuheshimu.

“Pia nishukuru mitandao ya kijamii na wanahabari kwa kuweza kufikisha ujembe, kama unavyoona mkutano wa leo umekuwa na majibu kwa baadhi ya changamoto,” amesema.

Pia amesisitiza kuwa amefurahi kuwaona wasanii maarufu kama Lulu na Ray kwa kuungana nao katika mkutano huyo.

Na Laila Sued na Salum Kaorata

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents