Michezo

Bodi ya Tenis yaomba radhi kwa udhalilishaji wa watoto

Bodi ya mchezo wa tenis nchini Uingereza imeomba radhi kwa kitendo cha udhalilishaji kilichofanywa na kocha, Daniel Sanders wa kituo cha kufundishia tenis cha Wrexham Tennis Centre.

Aliyekuwa kocha wa Wrexham Tennis Centre, Daniel Sanders 

Chama cha mchezo wa tenis nchini Uingereza  (LTA), kimesema kuwa kitendo kilichofanywa na kocha Sanders ambaye anatumikia kifungo cha miaka sita jela ni ishara tosha ya kuonyesha kuwa uwajibikaji wa kuwalinda watoto bado hautoshi.

Daniel Sanders, mwenye umri wa miaka 42, ameanza kuitumikia adhabu yake ya miaka sita jela tangu mwezi Julai baada ya kukutwa na hatia ya udhalilishaji wa kingono kwa watoto wadogo.

Bodi ya mchezo huo nchini Uingereza imesema kuwa nguvu iliyopo sasa ya kuwalinda watoto bado hatoshi na hivyo ni lazima kufanyike uchunguzi zaidi kwakile kilichotokea.

Sanders, aliyetokea Wrexham aliichezea klabu ya Tim Henman kabla ya kustaafu kwake mwaka 1996 na kuanza safari yake ya kufundisha mchezo huo wa tenis.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents