Michezo

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC yamteua, Salim Kikeke na kumpa jukumu hili Uingereza

Bodi ya Wakurugenzi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC imemteua Mtangazaji mashuhuri wa shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Salim Kikeke kuwa Balozi wa Simba Sports Club .

“Mboya ndiye mmoja kati ya rafiki zangu  ambao

Salim Kikeke ameteuliwa kuwa balozi wa Simba SC wa jiji la London nchini Uingereza katika tukio hilo mtangazaji huyo alikabidhiwa jezi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji.

Kikeke ni mtangazaji maarufu na mwenye kujadiliwa kila uchao huku umaarufu wake ukiwa sio tu Tanzania bali ni maeneo mengi ya Dunia hasa kunakozungumzwa lugha hadhimu ya Kiswahili.

https://www.instagram.com/p/B3Bwd7pHrYR/

Salim ni Mtanzania anayetangaza vipindi mbalimbali katika shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), huku safari yake ikianzia katika kituo cha TV cha CTN ambacho kilikuwa na radio kwa wakati huo ikifahamika kama Classic FM ambayo kwa sasa ni Magic FM.

Kisha Radio Tanzania (RTD) ambapo kwa sasa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kisha kuamia ITV na Radio One na ndipo Mwezi Mei 2003 akajiunga rasmi na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents