Habari

Bombardier Dash8-Q400 ya ATCL yafanyiwa ukaguzi angani

Ndege mpya moja kati ya mbili za shirika la ndege (ATCL), kwa mara ya kwanza imeruka kufanyiwa ukaguzi kwa mara ya kwanza kabla ya kuanza rasmi safari zake nchini.

3953347

Akizungumza kabla ya kuruka ndege hiyo, meneja wa kitengo cha dharura, John Chaggu, alisema ndege hiyo inaruka kwa mara ya kwanza kwa majaribio na kufanyiwa ukaguzi kabla ya kuruhusiwa rasmi na TCAA.

“Juzi tuliifanyiwa ukaguzi wa kuangalia namna ya kuwahudumia abiria na inapotokea dharura jinsi gani tutawahudumia na kuhakikisha wako salama,” alisema. “Hatua hiyo tumefaulu vizuri sana. Hii ya leo si ndege ya kibiashara, hatutabeba abiria wa aina yeyote zaidi ya watu wachache ambao wanahusika katika kufanya ukaguzi huu. Hii ya leo tunakwenda Kigoma baada ya hapo Mwanza halafu tunarudi tena Dar es Salaam,” alisema Chaggu.

Marubani wa kitanzania wakishirikiana na marubani wa kutoka Canada waliokuja na ndege hiyo kwa mara ya kwanza, walirusha ndege hiyo ikiwa ni hatua ya kufanyiwa ukaguzi na mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania (TCAA).

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents