Tupo Nawe

Bondia Amir Khan ambaye Mwakinyo anatamani kupigana naye, apigwa KO ya ajabu Marekani (+video)

Bondia Muingereza, Amir Khan amejikuta katika wakati mgumu na kushindwa kuendelea na pambano baada ya kupigwa ngumi maeneo ya sehemu nyeti (Low Blow) na mpinzani wake Mmarekani, Terence Crawford.

Kwenye pambano hilo la ubingwa ambalo limepigwa alfajiri ya kuamkia leo katika ukumbi wa Madison Square Garden Jijini New York Marekani, Crawford alionekana kutawala kwa muda wote mpaka raundi ya 6 alipomaliza pambano kwa kumtwanga KO Amir Khan.

Kufuatia kipigo hicho, Amir Khan ameomba radhi kwa mashabiki wake kwa kudai kuwa hakupenda kutoendelea na pambano lakini alijisikia maumivu makali sana.

Sikupenda kabisa kutoendelea na pambano lakini nilizidiwa na maumivu makali, nawaomba radhi mashabiki wangu, mchezo ulikuwa unavutia na ningependa kuendelea kama refa asingesitisha pambano kwa muda mfupi,“amesema Khan muda mfupi baada ya kumalizika kwa pambano hilo.

Amir Khan amekuwa akishambuliwa na mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii kwa kumuita ‘Biskuti’ hii ni kutokana na kuwa mwepesi pindi anapopigwa masubwi mazito.

Bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo kwenye moja ya mahojiano yake na Bongo5 alishawahi kukiri kuwa Bondia huyo ni dhaifu kwenye maeneo ya shingo na anatamani siku moja apambane naye.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW