Michezo

Bondia McGregor ashindwa kuzuia hisia zake kwa kocha wa Manchester United Ole Gunnar, ammwagia sifa kede kede

Mchezaji wa michezo ya boxing kutoka nchini Ireland Conor Anthony McGregor alimaarufu Conor McGregor, amejitokeza na kumsifia kocha wa sasa wa Manchester United Mnorway Ole Gunnar Solskjaer baada ya ushindi wa ugenini dhidi ya Arsenal.

Mkali huyo wa mchezo wa MMA amefunguka kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema kuwa:-


.
“Ole Gunnar Solskjaer ni mtu maalum! Super Sub ya Manchester United akiwa mchezaji na baadaye kocha”-baadhi ya maneno yanayotoka kwenye tweet ya McGregor. “

Ikumbukwa kuwa Manchester United tangu akabidhiwa Ole Gunnar tayari amecheza michezo 8 na kufanikiwa kushinda yote 8 huku akifunga zaidi ya magoli 20.

Lakini pia wakati Mourinho kocha wa zamani anafukuzwa timu hiyo ilikuwa nyuma kwa alama 8 na timu iliyoko nafasiya 5 na sasa zimefungana alama sawa timu iliyoko nafasi ya 5 na 6.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents