Michezo

Bondia, Ricky Burns atamba kumpiga Crolla wikiendi hii

Mwanamasumbwi, Ricky Burns ametamba kumpiga mpinzani wake Anthony Crolla katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi hii.

Pambano hilo la uzito wa lightweight litakalo fanyika Manchester Arena, Burns anaamini atawafurahisha mashabiki wake wakati atakapochukua ushindi mbele ya bingwa huyo wazamani wa dunia.

Mabondia wengi wamekuwa wakitamba kabla ya pambano lakini mwishowake hupoteza mchezo.

Alipoulizwa bondia huyo na Sky Sports nini atafanya kama atapoteza mchezo huo kwa kupigwa na Crolla amesema ” Siwezi kupoteza mchezo huo hivyo sitakujibu swali lako.”

“Mbele ya macho yangu nalitazama pambano hili kuwa gumu lakini nitahakikisha nachomoza na ushindi.”

Mabondia hao wote wawili wamepoteza mapambano yao ya mwisho kabla ya kukutana katika ulingo Jumamosi hii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents