BurudaniHabari

Bongo Fleva ni kama Siasa tu

Joh MakiniSi mashabiki wote wanaofahamu kuhusiana na mwanahipho Joh Makini anakotokea na sababu zipi zinazomfanya akomae kwa kunadi mkoa anaotokea katika kila tungo zake.

Joh MakiniSi mashabiki wote wanaofahamu kuhusiana na mwanahipho Joh Makini anakotokea na sababu zipi zinazomfanya akomae kwa kunadi mkoa anaotokea katika kila tungo zake.

“unajua wasanii wengi wanaotoka mkoani wakifika mjini wanakuwa kama wanaona noma kuelezea wanakotokea kutokana ufinyu wa akili zao ambazo huamini kuwa ukisema unatoka mkoa flani utaonekana mshamba na sio mjanja imeshajengeka kuwa mzawa wa Bongo ndio kuwa mjanja” alisema Joh Makini a.k.a Rapture.

Ni mzawa halisi mkoani Arusha na ndiyo sehemu ambayo amekulia na kusomea na ni kitu ambacho anapenda kila mshabiki wake alijue na kuliheshimu hilo.

Akizungumzia game ya Hip Hop hapa nchini anasema “muziki kwa kweli umejaa ubaguzi wa hali ya juu kwani kama ingekuwa kurekodi ndio kufanya vizuri nadhani ningekuwa miongoni mwa wasanii wa mwanzo kutoka mkoani Arusha kufanya vizuri kisanaa nchini, lakini wasanii wa hip hop hawapewi nafasi inayostahili wanabaniwa sana wakati muziki wa Bongo Fleva mimi nauona kama ni siasa kwani umejaa longo longo tupu” alisema Joh Makini.

Aliendelea kusema Joh “nafanya Hip hip na ndio muziki pekee ninaouzimia tangu nikiwa na umri mdogo sana lakini kabla sijaja Bongo ilikuwa ni ngumu sana kwa msanii kutoka A-Town na kufanya vizuri jambo ambalo lilishajengeka na kuleta imani ya kuwa wa mkoa hawajui kitu. Ndio maana katika tungo zangu napenda kusisitiza nakotokea ili kufuta dhana ya kuwa wapo wakali na sio Bongo peke yake”

Joh makini aliwahi kuwa mmoja kati ya wasanii waliokuwa chini ya lebo ya DownTown Records ambayo inamilikiwa na Prodyuza D-Money, lakini aliamua kuimwaga lebo hiyo baada ya kuona uongozi una mambo mengi kiasi kwamba alikuwa ni mtu kusubiri muda wote.

“nimeshazinguliwa sana na Maprodyuza wa studio mbali mbali na watangazaji wa redio za hapa jijini, lakini namshukuru mungu kwa kuniwezesha walau sasa naeleweka nafanya nini katika Hip hop ya bongo” alisema Joh Makini aliyewahi kutamba na vibao kama ‘hao, rusha miko juu’ na sasa anafunika na jiwe lake ‘Chochote Popote’ kilichorekodiwa na mandugu Digital.

Amesisitiza sana suala la wadau kijali maslahi yao na kudidimiza maslahi ya wasanii hasa wa Hip Hop ambao siku zote hawapati haki zao za kimsingi katika medani nzima ya muziki wa kizazi kipya, wawe waaminifu katika kuhakikisha sanaa ya kibongo inasimama.
Source: Bongo5

{mos_sb_discuss:6}


Bongo5.com brings you the latest news from East Africa at your finger tips. If you have a story you’d like to share please send an email to [email protected]

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents