Bongo Movie

Bongo Fleva wawalaza Bongo Movie

10_Kombe_likitolewa_kwa_kipa_wa_timu_ya_Bongo_Fleva_Tunda_Man_iliyoibuka_kwa_ushindi_wa_mbili_bila

 

Siku ya Jumamosi jioni, kulikuwa na mtanange wa kukata na shoka kati ya timu ya mpira wa miguu ya Bongo Fleva fC, na Timu ya Bongo Movie Fc, katika mechi ya Hisani ya kukusanya fedha za kuwasaidia wahanga wa maathiriko ya Mabomu Gongo la Mboto.


Katika mtanange huo, Bongo Fleva Fc iliibuka kwa ushindi wa bao mbili kwa zero, na yote hayo yalifungwa na H. baba ambaye alizitikisa kisawasawa nyavu ya wapinzani wao.

Mgeni rasmi alikuwa Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa na mbunge wa Kinondoni Idd Azzan, huku wakishirikisha na wananchi ambao walijaa kwa wingi ili kuja kupata burudani, pia kuchangia kiasi walichonacho kwa waathirika hao.

1_timu_ikiingia_uwanjani_zikiongozwa_na_viongozi_wao_wa_Bongo_fleva_Fc_na_Move_Fc

Timu zote mbili zikiingia uwanjani, kwa kuanza mtanange mzima.

2_Timu_ya_Move_Fc_zikiwa_katika_picha_ya_pamoja_kabla_ya_mechi_kuanza

Timu ya Bongo Movie Fc, ikiwa imejipanga katika picha ya pamoja kwaajili ya kupata kumbukumbu.

4Mgeni_meya_wa_jiji_Slaa_rasmi_akimpa_mkono_Yusuph_Mlela

Mgeni rasmi Jerry Slaa akimsalimia  Yusuph Mlela, wakati wakuanza kwa mechi hiyo.

4_Tunda_Man_Katikati_akiwa_kama_kipa_akimtambulisha_mgeni_rasmi_Slaa_kwa_kocha_wa_timu_yake_Bongo_fleva_Fc_Joseph_Haule_Prof_J

Kipa wa Bongo Fleva akimtambulisha mgeni rasmi Jerry Slaa  kwa kocha wake, Prof Jay

5_Mammbo_yalikuwa_kama_hivi_chenga_kwenda_mbele

6_goli_la_pili_lililofungwa_na_H._Baba_likiingia_nyavuni

Goli la pili alilofunga H. baba hapa likiingia nyavuni.

7_Mazoezi_yakiendelea_Masanja_na_Jb

Mikwara ya Jb na Masanja kwa kuzunguka uwanja, hatmaye wakawa hoi na kuanza kuanguka kiwanjani.

8_Kanumba_akiwa_haamini_kama_kweli_amekosa_namba_ya_kucheza

Kanumba akiwa haamini kama kweli amekosa kucheza mechi hata kidogo, ingawa alimbembeleza refa, lakini aliambiwa ‘Sub’ imeisha na haiwezekanai kuingiza tena.

9Wageni__rasmi_wakiwa_wametulia_kusubiri_kutoa_zawadi_kwa_mchezaji_bora_na_timu_iliyoshinda

Mgeni rasmi akiwa anasubiri timu ya kuipa kombe.

H.baba_akielezea_ushindi_walioupata_kwa_kufunga_magoli_magoli_mawili_peke_yake

H.baba akieleza jinsi gani alivyoweza kuliza Bongo Movie, ingawa yeye mwenyewe anaimba nakuigiza.

Makocha_wakiwa_katika_picha_yaa_pamoja

Marefa walioendesha menchi nzima wakiwa katika picha ya pamoja, walichezesha mpira kwa amani na bila ya upendeleo wakijua kabisa kama hii ni burudani tu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents