Bongo Movie

Bongo Movie Kufanya Uchaguzi Wa Viongozi Nov 30 Lamada Hotel

ISSA MUSSA WILLIAM MTITU NA JB
Uongozi wa Bongo Movie umejipanga kufanya uchaguzi wa viongozi ambao utafanyika tarehe30 November katika ukumbi wa Lamada Hotel . Bongo5. com imefanikiwa kuongea na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa Bongo movie Jimmy Mafufu na kuambiwa kuwa mchakato wa uchaguzi unaendele vizuri kwa sababu watu wameshaanza kuchukua form za nafasi mbali mbali za uaongozi katika chama hicho.
Bwana Mafufu alisema “maandalizi ya uchaguzi yanaendelea vizuri sana na uchaguzi utafanyikia pale Lamada Hotel na tumepanga Uchaguzi utafanyika kuanzia saa 5 asubui na watu ambao wataweza kuchagua Viongozi ni wale wanachama ambao wamejiunga na Bongo Movie, nani wanachama ambao wanatambulika na bongo movie na wapiga kura wote watakuwa na card kama hauna ina maana hauta ruhusiwa kupiga kura”.
Wale ambao wanahitaji kuwa wanachama wa Bongo Movie ili waweze kupata nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka inatakiwa waje wachukue form za Uanachama ambazo zinapatika pale Maisha club,au wanaweza wakamuona Mayasa Mrisho na Jimmy Mafufu ili kupata form hizo kwa wakati ili mujiwekee nafasi ya kuchagua kiongozi mnaemtaka hapo tarehe30 pale Lamada Hotel.
Bwana Mafufu alitoa angalizo kwa vyombo vya habari kwa kusema ushirikiano wa vyombo vya habari kwa Bongo Movie ni mdogo sana na kushangaa pale wanapofanya mambo mazuri ambayo jamii inatakiwa kujua, media huwa hawaandiki ila inapotokea mmoja wao kafanya jambo baya wanakuwa wa kwanza kuliandika kwa kuwa ni baya, hatukatai, kwamba huwa hamuandiki mambo yetu , bali mnapenda sana kuandika udaku mwingi na kuacha mambo mengi ya msingi.
Napenda kurudia na kusisitiza tumefanya mambo mengi mema ambayo hamjayaandika alafu mnakuja mbele na kusema Bongo Movie wote wakati ni wachache tu, kati yetu, ambao wamehusika na tukio kama hilo.
Anakumbushia kwa kusema “nakumbuka tukio lile baya la Aunt Ezekiel wakati wa shoo za Fiesta, sisi kama Bongo Movie hatukupenda, na pia baadhi ya vyombo vya habari vilitujumuisha Bongo Movie wote, wakati sisi Bongo Movie tulikaa chini na kutoa adhabu kwa Aunt Ezekiel asijihusishe na kitu chochote katika uigizaji hata kushirikishwa katika muvi yeyote kwa muda wa miezi sita.
Adhabu ile ilionyesha ni jinsi gani tulivyo makini, sasa vyombo vya habari vya udaku ambavyo kila siku wamekuwa wakiandika mabaya kwa Bongo movie inabidi wabadilike ili kutupa nafasi ya kuonyesha mazuri yetu ambayo jamii inatarajia tukiwa kama kioo cha jamii

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents