Bongo Movie

Bongo Movie tuna vitu vikubwa lakini sijui tunakosea wapi – Faiza Ally

Msanii wa filamu Bongo, Faiza Ally amesema tasnia hiyo ina vitu vikubwa ila hajui ni wapi inakwama kwa sababu ushirikiano na umoja wanao.

Muigizaji huyo ameeleza hayo kufuatia ushirikiano ulionyeshwa na waigizaji wenzake katika mazishi ya video vixen, Agness Gerald ‘Masogange’ ambaye alizikwa jana mkoani Mbeya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza ameandika;

“Tunaishi kwa kujifunza na mara nyingi mitazamo ya nje sio halisi, naomba nimpongeze IreneUwoya kwa kuwa rafiki mwema a special kipindi hiki, nimemuona akishiriki na kwenye utulivu sana yaani kasimama kama rafiki na hivi ndio inavyo takiwa, yaani jambo linapo kufika la mtu wa karibu sio kulia sana au kupoteza fahamu lazima usimame ujue hatma ya mwenzio kwanza,” amesema.

Aliendelea kwa kuwapongeza Zamaradi Mketema, Steve Nyerere, Aunty Ezekiel, Husna Maulid, Husna Sajent, Shilole kwa kusimamia vizuri tukio hilo vizuri.

“Nahisi Bongo Movie tuna vitu vikubwa sana wote kwa pamoja lakini sijui tunakosea wapi, maana kwa ushirikiano huo huo wa msibani, urudi kwenye kwenye kazi naamini kuna hatua kubwa sana tutapiga, nisema tu mpo vizuri sana, nyinyi ni wa maana sana,” ameongeza.

Hapo jana April 23, 2018 alizikwa Agness Gerald ‘Masogange’ ambaye alikuwa video vixen na muigizaji wa filamu, Masogange alifariki April 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents