Bongo Movie
Bongo Movie waja na filamu ya Rais Magufuli
Kundi la filamu la Mkoa wa Shinyanga lifahamikanalo kama “Bongo Movie Shinyanga’ wameandaa filamu fupiĀ itakayo lenga kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua anazozifanya katika kulinda rasilimali za nchi.
Kupitia Mwenyekiti wa kundi hilo Juma Songoro ameeleza kuwa “Mkoa wa Shinyanga wanampongeza Rais na wameaanda filamu fupi ambayo ni zawadi kwenda kwa Rais kwa jitihada anazozichukua katika kulinda rasilimali za nchi ikiwemo madini.”
Filamu hiyo fupi imepea jina la ‘Tanganyika karne ya 18’ na inaonyesha nchi za nje jinsi wanavyoiba madini kutoka Tanzani.
https://youtu.be/YMzEGxADePw
Na Laila Sued