Bongo MovieBongo5 Makala

Bongo Movies wana allergy na James Bond?

Usiku wa Alhamis pale Mlimani City jijini Dar es Salaam ulikuwa wa kihistoria kwa wapenzi wa filamu za James Bond aka 007. Heineken waliwezesha uzinduzi wa kipekee wa filamu mpya ya mpelelezi huyo iitwayo Skyfall.

Kama ulisoma habari yetu ya jana kuhusiana na uzinduzi huo, wengi walifurahishwa na Skyfall kutokana na kuwa na action za kufa mtu japo kifo cha bosi wa James Bond (Daniel Craig) kilichawasikitisha wengi na kuanza kuwaza ni nani atakayeziba pengo hilo japo filamu imeisha kwa 007 kukabidhiwa mikoba ya kukishikilia kitengo cha secret service kilichokuwa chini M.

Baada ya filamu kuisha, crew yetu iliwahi nje kutaka kupata picha za wote waliohudhuria uzinduzi huo. Kulikuwa na watu wa kila aina katika tasnia ya burudani nchini kuanzia Salama Jabir, Master Jay, Rita Paulsen, Lady Jaydee na mumewe Gadner G Habash, AY, Dj Fetty, Izzo B, Quick Rocka, Jokate Mwegelo, Vanessa Mdee, Nancy Sumari, Nchakalih, B12 na wengine wengi ambao list yake inaweza ikamaliza ukurasa mzima.

Lotus, Vanessa Mdee na Abby

Lakini kulikuwa na kundi muhimu la watu ambao tulitegemea kuwakuta, watu wa Bongo Movies. Camera zetu zilijaribu kuangaza kama zingeweza kunasa sura za watu kama Vincent Kigosi, Irene Uwoya, JB, Jackline Wolper na wengine kwenye tasnia ya filamu nchini lakini hazikuona hata mmoja.

Kwa haraka haraka tulianza kujiuliza ina maana hakuna hata staa mmoja wa filamu aliyealikwa kwenye uzinduzi huo? Kama Heineken haikufanya hivyo basi lawama tuwatupie wao japo hatutaki kuamini hivyo. Ni hakika kuwa kulikuwepo na mwaliko wa waigizaji wawili watatu wa Bongo Movies ambao wangewakilisha wenzao.

Tunasitika kuona kuwa watu waliotakiwa kuwa wa kwanza kwenda kwenye uzinduzi kama huo waliamua kufanya mambo yao. Hiyo ilikuwa ni fursa nzuri kwao kujifunza mengi yatakayosaidia kuboresha filamu za Tanzania. Kwa walioiangalia filamu hiyo, kuna mengi walijifunza ambayo yangeweza kutumika kama mfano kwenye filamu zetu.

Tunafahamu kuwa wapo waigizaji makini nchini ambao huwa mbele katika kufuatilia filamu mpya za nje ili kuona kuna kitu gani kipya katika tasnia hiyo kwakuwa kila siku mambo yanabadilika. Lakini pia wapo waigizaji wa nyumbani ambao huishia kuangalia filamu za Nigeria tu na hivyo kushindwa kupanua upeo wao katika umahiri wa uigizaji wa kisasa. Hilo ndio suala linalosababisha filamu nyingi za Tanzania kuwa na mada za aina moja.

Tuwape sifa wasanii wa muziki nchini ambao kama ulibahatika kwenda kwenye show ya Fiesta ya Dar es Salaam iliyoongezewa utamu na Rick Ross, wengi walihudhuria hata wale ambao hawakuwa kwenye ratiba ya kutumbuiza.

Lengo la wengi lilikuwa ni kwenda kuona rapper mkubwa kama Rick Ross huwa anafanyaje kwenye stage. Wasanii makini walijifunza kitu. Hivyo tunauliza, wasanii wa filamu nchini hawakutaka kujifunza chochote kutoka kwenye uzinduzi wa Skyfall uliokuwa umetengazwa kwa muda mrefu tu? Ama wana allergy na filamu za James Bond?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents