Bongo Movie

Bongo na filamu za mafungu

filamu_zetu_face
Soko la filamu kwa sasa linaonekana kukua kadri siku zinavyozidi kwenda lakini pia wizi wa kazi za wasanii hao kila siku nao unazidi kukuwa, kiasi cha wasanii kuwa na filamu kumi au ishirini lakini hana hata nyumba wala gari.

 

Hapo ndipo ninapojiuliza maswali mengini, miongoni mwa maswali ninayojiuliza huenda hata wewe unaweza kujiuliza na kujipatia majibu, au usijipatie mwenyewe lakini kuna mtu akakupatia kuhusiana na huu wizi wa waziwazi kwa kazi hizo za wasanii.

kwanza najiuliza hivi filamu za Tanzania zinalipa mpaka kiasi cha kuuza filamu moja shilingi mia tano, yaani mbili au tatu shilingi elfu moja ‘1000’?

Pia najiuliza kama ndiyo mbona wanalalamika, au ndiyo Watanzania watu wa amani, hivyo  kila mmoja apate ridhiki kutokana na kazi zake, na usimsumbue mwenzako hata kama anachakachuaji kazi zako? Pia najiuliza hivi hizi Cd zinazounzwa mafungu hawazioni, na kama hawazioni mbona zinauzwa sehemu za wazi kama Ubungo, Kariakoo, Manzese, na kila sehemu yenye mkusanyiko wa watu wengi? kuna muda ninafikiri  huenda yakawa ni  makubaliano kati ya mwenye filamu na mchuuzi wa kutengeneza Cd feki, lakini kwa nini wengine wanapigana na mauzo haramu na wengine wanakodoa macho kuangalia kama hawahusiki?

Kweli mwananchi anaweza kumtetea msanii ambaye hajitetei kwa kununua Cd Original kwa kuachana na feki, wakati Oroginal ni shilingi 5000, mpaka 3500 kwa Cd mmoja, na Cd mbilli feki ni shilingi 1000 na ukiangalia ndani Movie ni ile ile na inaonyesha vizuri? Kuna muda nasema hivi hawa wachakachuaji wananguvu kiasi gani? hivi nguvu zao zinazidi wasanii wenye mali zao, au zinazidi kitengo cha kudhibiti kazi za wasanii COSOTA?

Jamani hata kama kweli mnapata faida, hivi kweli inalipa kiasi cha kuachia kazi zinaibiwa kirahisi namna hii, au ndiyo Serikali haijasimamia? Wakati wenzenu wanaambiwa wachonge barabara kwa majembe Serikali italeta vifusi na rami, kwanini nyinyi hamtaki kutengeneza barabara yetu ili Serikali iwaletee rami?

filamu_zetu

Au mnaamini kazi zenu zikiingia mtaani kwa wingi basi umaarufu utaongezeka kwa kuwa mtajulikana kwa wepesi? Basi kama hamna meno kutoka Serikalini basi jaribuni kubana hata kwa fizi…………… Wacha niishie hapa labda na nyinyi mtajiuliza, kwanini filamu mpya inatangazwa itatoka lakini kwa wachakachuaji tayari imeshatoka kwa bei ya buku moja ‘1000’…

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents