Umbea

Bongo5 Gossip: Mr. Nice Apigana Bar


Msanii maarufu wa muziki wa Takeu Lukas Mkenda maarufu kama Mr Nice, ambaye amerudi kwenye game kwa kasi kupitia wimbo wake wa ‘Tabia Gani’, jana usiku alitwangana makonde live na jamaa mmoja ambaye alisadikika kwa jina la John.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambalo lilitokea mida ya saa sita usiku katika baa ya Uhuru Peak iliyopo maeneo ya Mango Garden kinondoni Vijana, Mr Nice alifika eneo hilo na kumkuta kijana huyo akiwa ameketi akienjoy na washikaji zake.

Baada ya kusalimiana,Mr Nice alimkashifu kijana huyo kwa kumwambia “ Wewe bia nikununulie na bata nikupe alafu baada ya hayo yote unamtongoza dem wangu??”.
Baada ya kusema hayo kijana Yule alikana kufanya kitendo hicho ambapo nice alijaribu kumpigia simu dem wake lakini hakupokea.

Wawili hao waliendelea kurushiana maneno baada ya demu wa Nice kutopatikana, Mr Nice aliendelea kumsakama yule kijana John ambaye nae alimjibu kwa nyodo na jeuri kuwa hawezi kumchukua dem wake kwani hataki kufa na pia akmwambia nice atafute historia ya familia yao ambapo nice alimjibu asiingize familia yake kwani yeye anataka ajiongelee mwenyewe.

Shuhuda huyo aliendelea kusema baada ya kuambiwa hivyo bwana John alimwambia Nice kwamba kwa sasa yeye nice amechoka na wala asijifananishe nae na pia awaulize washkaji zake ambao wanamjua vilivyo. Maneno hayo hayakuonekana kumuuma Mr Nice ambaye alionekana kumpuuzia bwana John.

Hivyo Nice alikuwa anaelekea kaunta ambapo John alitupa kijembe kingine kwamba hawezi kushea demU naye Nice kwani dem mwenyewe ni m&*#@, kauli hiyo ilimfanya Nice kurudi na kumwasha makofi, jambo hilo lilifanya watwangane makonde kwa dakika kama 3 hadi hapo mabaunsa na watu wengine walipoingilia kuwatenganisha.

Bongo5 inaahidi kumtafuta Nice ili aeleze kwa undani sakata hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents