Burudani

Boomplay waingia makubaliano na Universal Music Group ya kusambaza muziki barani Afrika

Universal Music Group inakuwa kampuni ya kwanza kuingia mkataba na jukwaa linaloongoza kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki barani Afrika la Boomplay.

Boomplay huduma ya muziki inayoongoza upande wa kusikiliza na kupakua muziki barani Afrika kushirikiana na Universal Music Group (UMG), kampuni inayoongoza katika usambazaji wa muziki ulimwenguni, leo wanatangaza kusainiwa kwa makubaliano ya kibali cha kusambaza muziki katika masoko mengi ndani ya Afrika.

UMG ni kampuni ya kwanza ya muziki wa kupitisha leseni yake kwa Boomplay, ambayo inajulikana kwa huduma yake ya kusikiliza muziki barani Afrika. Chini ya makubaliano ya mkataba huu wa miaka mingi na ufanisi mara moja, Boomplay itasambaza muziki kutoka kwa UMG nchini Tanzania pamoja na Nigeria, Ghana, Kenya, Rwanda, Uganda na Zambia.

Mpaka sasa, Boomplay ina nyimbo zaidi ya milioni mbili na maelfu ya video zinazopatikana kwa watumiaji wake zaidi ya milioni 36, na watumiaji karibu milioni mbili wanaoongezeka kila mwezi.

Watumiaji wa Boomplay sasa wanaweza kupata nyimbo za nyumbani na za kimataifa kutoka UMG wakiwemo wasanii kama Eminem, Tekno, Post Malone, Nicki Minaj, Lady Zamar, Lil Wayne, Bob Marley, Brenda Fassie, Wurld, J.Cole, Dr. Tumi, Nasty C, 6lack, Diana Ross, Hugh Masekela, Jon Bellion, Larry Gaaga, Tamia, Maroon 5, Aka & Anatii, TJAN, Jah Prayzah, Nonso Bassey, Mafikizolo, Cina Soul, Ella Mai, Mr. Eazi na wengine wengi.

Mapema mwaka huu, UMG ilitangaza uzinduzi wa Universal Music Nigeria, ikiwa na lengo la kuwapa wasanii fursa nyingi barani Afrika kwa ajili ya kufanikisha kazi zao kufika hatua za kimataifa. UMG inaendelea kusukuma gurudumu la lengo lao la kukuza mazingira ya muziki wa Afrika pamoja na kurekodi muziki, kuchapisha muziki, uzalishaji, matamasha, ushirikiano wa makampuni na jitihada za biashara.

Katika hili, Makamu wa Rais wa Universal Music Group, idara ya Maendeleo ya Masoko, Adam Granite alisema, “Tunatarajia kufanya kazi na Boomplay ambapo tutawawezesha wasanii wetu wa Kiafrika kuwa wabunifu, jukwaa la masoko na uendelezaji wa rasilimali ili kuharakisha kazi zao zinaendelea kukua barani Afrika. Mkataba huu utasaidia wasanii wa UMG kufikia watumiaji wapya, huku wakiongeza hamasa ya usikilizaji wa muziki wa Afrika ili watapate faida kuwafikia mashabiki wa muziki, wasanii wengine na wazalishaji muziki.

“Ushirikiano huu utaendelea kufikia watu wengi na kuhakikisha kazi za wasanii wetu zinawafikia mamilioni ya wapenzi wa muziki barani Afrika,” alisema Ezegozie Eze Jr., Meneja Mkuu wa Universal Music Nigeria, “Tunafurahia kuwa kampuni ya kwanza ya muziki kushirikiana na Boomplay na tunatarajia kuleta ubunifu wa hali ya juu kwa wasanii wetu na kwa watumiaji wengi Afrika. ”

Akizungumza pia, Mkurugenzi Mtendaji wa Boomplay, Joe He, alisema kuwa Boomplay itaendelea kuunda ushirikiano unaoimarisha mfumo wa kidigitali na kuunganisha wapenzi wa muziki na nyimbo wananazozipenda wakati wowote na mahali popote.

“Boomplay imejizatiti kuendelea kutengeneza shauku kubwa ya muziki wa kiafrika katika njia halali, hasa kwa watumiaji wa Boomplay kushirikiana na lebo kubwa za muziki duniani kama Universal Music Group inatoa nafasi nyingine kubwa kwa sisi kufanya hivyo “,
alisema.

App ya Boomplay ambayo kwa sasa inapatikana kwa watumiaji wa simu za Android, inatarajia kuzindua app kwenye jukwaa la iOS hivi karibuni. Kwa kuongeza, watumiaji wapya wa Boomplay wataweza kupata usajili wa miezi moja bila malipo pale watakapojiunga na kifurushi cha mwezi mmoja kinachojirudia.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na

Universal Music Group:
James Murtagh-Hopkins / +44 203 932 6822 [email protected]

Boomplay:
Tosin Sorinola / +234 8166896617 [email protected]
Natasha Stambuli / +255 677007428 [email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents