Burudani

Bosi wa Candy & Candy Joe asomewa mashtaka akiwa Hospitali

Bosi wa kampuni ya Candy & Candy, Joe Kairuki Jumatatu hii mkoani Arusha amesomewa mashtaka ambayo yanayomkabili huku akiwa amelazwa katika hospitali moja iliyopo mkoani humo.

Mwanasheria wake John Malya, alisema Joe alikamatwa baada ya kesi yake ya awali kutupiliwa mbali na mahakama ya Arusha, kisha kukamatwa tena nje ya mahakama.

Taarifa za awali zinadai Joe alikamatwa Julai 2 mwaka huu na kutupwa rumande huku kukiwa hakuna ndugu wala rafiki aliyekuwa anafahamu alipo.

“Baada ya kufikishwa mahakamani shauri lake lilifutwa juzi kisha polisi walimkamata nje ya mahakama na kumpeleka kituo cha polisi Longido ambako anashikiliwa,”alisema Malya.

Mpaka sasa Joe bado yupo hospitali kwa matibabu zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents