Habari

Bosi wa vyombo vya habari mbaroni kwa tuhuma za kula njama na nchi za kigeni Hong Kong 

Mfanyabiasha maarufu na mmiliki wa vyombo vya habari wa Hong Kong, Jimmy Lai, amekamatwa hii leo kwa tuhuma za kukiuka sheria mpya ya usalama wa taifa.

Hong Kong Publisher Jimmy Lai Is Arrested Under National Security ...

Watoto wake wawili wa kiume na wakurugenzi kadhaa waandamizi wa kampuni inayochapisha magazeti yake, nao pia wamekamatwa.

Polisi ya Hong Kong imethibitisha kupitia Twitter kwamba imewakamata watu saba kwa tuhuma za kukiuka sheria hiyo mpya.

Polisi wamesema kuwa makosa yanayoshukiwa ni pamoja na kushirikiana na nchi za kigeni na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea.

Sheria hiyo mpya ya usalama wa taifa iliyoanzishwa na China ilianza kutumika mwishoni mwa mwezi Juni, na inawalenga wale wanaotaka kujitenga, vitendo vya ugaidi, mapinduzi na kushirikiana na vikosi vya kigeni. Adhabu ya makosa hayo ni kifungo cha hadi miaka 10 jela.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents