Habari

Boti za silaha za Iran zaitia tumbo joto Uingereza, yatishia kulipiza kisasi kwa kushikiliwa meli zake za mafuta 

Maboti ya Iran yaliyosheheni silaha yameripotiwa kujaribu kuzuwia safari ya meli ya mafuta ya Uingereza katika eneo la kuwa maji la Strait of Hormuz – kabla ya ya kufukuzwa na meli ya kikosi cha majini cha Uingereza.HMS MontroseHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMeli ya kijeshi ya Uingereza HMS Montrose imeripotiwa kuifukuza mbali maboti ya Iran

Taarifa za vyombo vya habari zimenukuu maafisa wa Marekani wakisema kuwa meli hiyo ya mafuta iliambiwa isimame katika maji ya Iran yaliyopo karibu ,lakini ikarudi nyuma na kuondoka baada ya onyo kutolewa na mele ya jeshi ya Uingereza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Iran imekuwa ikitishia kulipiza kisasi kufuatia kushikiliwa kwa moja ya meli zake za mafuta ambayo ilitekwa karibu na ibraltar wiki iliyopita.

Makao makuu ya wizara ya Ulinzi nchini Marekani Pentagon yamesema kuwa yanataarifa juu ya tukio hilo lakini hayakutoa taarifa zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa , boti tano zinazoaminiwa kumilikiwa na jeshi la Iran Iranian Revolutionary Guard ziliikaribia meli ya mafuta ya Uingereza ilipokuwa ikiondoka eneo la Ghuba.Ramani ya Straits of Hormuz na Bab al-Mandab

Image captionRamani ya Straits of Hormuz na Bab al-Mandab ambapo meli ya mafuta ya Uingereza inadaiwa kukabiliwa na maboti ya ya Iran

Wakiwa na silaha juu ya meli ya kijeshi ya Uingereza -HMS Montrose, wanajeshi wa kikosi cha majini wa Uingereza waliripotiwa kuzilazimisha boti za Iran kurudi nyuma . Waliafiki onyo na hapakuwa na makabiliano yoyote ya silaha.

Wiki iliyopita, Kikosi cha wanamaji cha Uingereza- British Royal Marines kilisaidia maafisa wa Gibraltar kukamata meli ya mafuta ya Iran kutokana na ushahidi kuwa meli hiyo ilikuwa inaelekea kwenye mwambao wa Syria ambao uko chini ya maneneo yaliyowekewa vikwaza na Muungano wa Ulaya.

Afisa wa Iran alisema kuwa meli ya mafuta ya Ungereza lazima ikamatwe na kama ikikamatwa haiwezi kuachiliwa.

Iran pia ilimuita balozi wa Uingereza mjini Tehran kumlalamikia juu ya kile ilichosema kuwa ni “aina ya uharamia”.

Na Jumatano rais wa Iran Hassan Rouhani aliikemea Uingereza, na kuitaja kama taifa lenye “uoga” na “lisilo na matumaini” kwa kutumia meli zake za kijeshi kuficha meli yake ya mafuta katika eneo la Ghuba.

meli ya kijeshi ya Uingereza HMS Montrose ilikuwa imeikinga meli ya mafuta Pacific Voyager ilipokuwa ikisafiri kuelekea katika maeneo ya Strait of Hormuz, lakini safari hiyo ilimalizika bila tukio lolote.Meli ya mafutaHaki miliki ya pichaREUTERS

Image captionMeli ya mafuta inashukiwa kubeba shehehena ya mafuta ghafi kuelekea nchini Syria

Mzozo wa hivi karibuni unakuja wsakati hofu ikiendela kutandabaina ya Marekani na Iran

Utawala wa Trump ambao tayari umejiondoa kwenye makubaliano ya kimataifa juu ya mpango wa nuklia wa Tehran – umeimarisha vikwazo vya kuiadhibu Iran.

lakini washirika wa Ulaya, ikiwemo Uingereza, hawakufuata mkondo huo wa Marekani.

Hata hivyo, uhusiano baina ya Uingereza na Iran umeendelea kuzorota, baada ya utawala wa Iran ”ulipojaribu kushambulia meli mbili za mafutra za Uingereza mwezi Juni.

Uingereza pia imeishinikiza Iran kumuachiliwa huru mama Muingereza mwenye asili ya Iran Nazanin Zaghari-Ratcliffe ambaye alikamatwa mnamo mwaka 2016 baada ya kupatikana na hatia ya ujasusi, ambao anaukana.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents