Habari

Brad Pitt: Kulea watoto sita sio kazi ndogo


Muigizaji wa filamu nchini Marekani, Brad Pitt amekiri kuwa kazi ya kulea watoto sita ni ngumu kuliko hata kuigiza filamu za action.

Watoto wa Brad na Angelina Jolie ni Maddox, 11, Pax, 9, Zahara, 7, Shiloh, 6, na mapacha wenye miaka minne Knox na Vivienne.

Muigizaji huyo amesema kazi ya ulezi ya watoto hao humpa shida kuliko hata stunts anazozifanya wakati wa uigizaji wa filamu za action ikiwemo filamu yake mpya ya ‘Killing Them Softly’.

“Getting the kids ready for school is every bit as painful as anything I had to do in this film,” alisema.
Kwa sasa Brad na Angelina wapo kwenye mchakato wa kuandaa harusi yao japo muigizaji huyo amesema rafiki yake kipenzi George Clooney hawezi kuwa mpambe wake kwakuwa haamini katika muungano wa ndoa.

Brad amesema bado hajapanga tarehe rasmi ya harusi yao ingawa watoto wao anawasukum;ua wafunge ndoa mapema.
Harusi yao inaweza kufanyika nchini Uingereza wakati huu wa majira ya kiangazi ambayo wanayatumia kupumzika jijini London.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents