Burudani

Brad Pitt na Angelina Jolie wapanga kuongeza mtoto mwingine wa kuasili (adoption)

Brad Pitt na Angelina Jolie wanadaiwa kuwa na mpango wa kuongeza tena familia yao kwa kuasili mtoto. Wapenzi hao tayari wana watoto sita – watatu wa kuasili na watatu wa kuzaa wao wenyewe.

rs_1024x759-130515132648-1024.JoliePittKids4.mh.051513

Chanzo kimoja kimeliambia jarida la Grazia kuwa “Angelina na Brad wametumia muda wao mwingi wa mapumziko kujadiliana kuhusu kuongeza familia”. Awali walidaiwa kutaka kuchukua mtoto huko Jordan, lakini mchakato ulikuwa mgumu hivyo wamedaiwa kuwa kwenye mazungumzo na kituo cha watoto yatima cha nchini Ethiopia.

Pitt na Jolie, wanajenga kliniki ya Ukimwi yenye jina la mtoto wa Zahara nchini Ethiopia na wanatarajiwa kwenda nchini humo mwezi April.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents