Burudani

Brandy apoteza fahamu ndani ya ndege

Msanii Brandy amejikuta katika wakati mgumu baada ya afya yake kutetereka akiwa kwenye ndege ya Delta Air Lines iliokuwa ikitokea New York kwenda Los Angeles.


Brandy

Muimbaji huyo alizimia ghafla katika ndege hiyo ndipo abiria wenzake wakatoa taarifa kwa wahudumu wa ndege ili aweza kusaidiwa kabla ya kupelekwa hospitali. Kwa mujibu wa TMZ, Brandy alitoa taarifa ya kujisikia vibaya kabla ya kupata tatizo hilo la kuzimia.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa imeeleza kuwa msanii huyo alipatwa na tatizo hilo kutokna na uchovu wa kazi nyingi, lakini aliruhusiwa kutoka hospitali na kurudi nyumbani baada ya afya yake kuonekana kuendelea vizuri.

“Brandy has been released from the hospital and is now at home resting. She has been traveling extensively as part of an ongoing tour and several personal appearances. In recent days she has taken more than 10 long haul flights including internationally. She was in the studio all night last night until it was time for her to leave for the airport to catch a 5:45 am flight” imesema taarifa hiyo.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents