Michezo

Brazil 2014: Samir Nasri na Gael Clichy waachwa kwenye kikosi cha awali cha Ufaransa

Kiungo wa Manchester City, Samir Nasri na beki wa pembeni Gael Clichy, wameachwa katika kikosi cha awali cha timu ya taifa ya Ufaransa ambacho kitaaanza kujiandaa na fainali za kombe la dunia za mwaka huu.

Samir Nasri & Gael Clichy_full

Kuachwa kwa kiungo Samir Nasri kumehusishwa na sakata la utovu wa nidhamu ambalo lilijitokeza wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2010. Kwa upande wa Gael Clichy ametemwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa, kutokana na kutopata nafasi katika kikosi cha klabu ya Man City, ikilinganishwa na wachezaji wengine waliotajwa katika nafasi ya ulinzi watakaokwenda nchini Brazil.

Kikosi cha wachezaji 23 kinachounda timu ya taifa ya Ufaransa tayari kwa fainali za kombe la dunia huko nchini Brazil ni pamoja makipa Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Steve Mandanda (Marseille), Mickael Landreau (Bastia). Mabeki: Mathieu Debuchy (Newcastle), Lucas Digne (Paris St-Germain) Patrice Evra (Manchester United), Laurent Koscielny, Bacary Sagna (both Arsenal), Eliaquim Mangala (Porto), Mamadou Sakho (Liverpool), Raphael Varane (Real Madrid).

Viungo: Yohan Cabaye, Blaise Matuidi (both Paris St-Germain), Clement Grenier (Lyon), Rio Mavuba (Lille), Paul Pogba (Juventus), Moussa Sissoko (Newcastle), Mathieu Valbuena (Marseille).

Washambuliaji: Karim Benzema (Real Madrid), Olivier Giroud (Arsenal), Antoine Griezmann (Real Sociedad), Loic Remy (QPR – on loan at Newcastle), Franck Ribery (Bayern Munich), Stephane Ruffier (Monaco).

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents