Tupo Nawe

Brazil ilivyopagawa na upasuaji wa kubadili sura (Plastic Surgery)

Wanaume nchini Brazil wameendelea kwa kasi kubadilisha nyuso zao kwaajili ya urembo au kuonekana na sura nzuri.

human-ken-doll-plastic-surgery-rodrigo-alves

Mtaalam mmoja wa masuala ya upasuaji nchini humo anasema, Kwa nyongeza ni kwamba kumekuwa na idadi kubwa ya vijana wengi wa kiume kufanya upasuaji kwa ajili tu ya urembo. Vijana wengi wamekuwa wakifanya upasuaji wa kuondoa mafuta kwenye matiti wale ambao wana vifua vikubwa, wengine kuondoa mafuta mwilini hasa wale ambao ni wanene na wengine wakifanya upasuaji ili kuweza kurekebisha mwonekano wa macho yao.”

Upasuaji huo ambao uliwagharimu watu maarufu kama Michael Jackson, huko Brazil hali imeongezeka zaidi kutoka watu 72,000 kwa mwaka hadi watu 276,000 kutoka 2009 hadi 2014.

Hii ikiwa inamaanisha kuwa kila saa moja kuna watu 31 wanafanyiwa upasuaji huo. Inasemakana duniani nchi hii ya Brazil inaongoza kwa upasuaji wa namna hii wa watu kubadilisha muonekano wao wa sura na mwili pia.

Rodrigo Alves

Wateja wengi wa huduma hii ni wa miaka kati ya 20 hadi 50. Ingawa wengi wanatoka katika mazingira ya kazi hivyo kuongeza idadi kubwa. Wengine wenye umri mkubwa hufanya upasuaji huo ili waweze kuendana na wapenzi wao kusionekane tofauti katika mwonekano wao hasa wanapokuwa wanatembea mitaani na hata picha zao kwenye mitandao ya kijamii.

“Wengi wao hawapendi kuonekana kwamba wanasura zilizochoka, hii pia imeathiri vile vile soko la ajira hapa Brazil,” anasema Mkurugenzi wa SBCP ambalo ni shirika linalofanya upasuaji huo lililozinduliwa rasmi mwaka 1948 katika Jiji la Sao Paulo. Kuna madaktari karibu 5,200 ambao ni wataalamu katika upasuaji wa aina hiyo.

Kijana mmoja, Rodrigo Alves, 31 aliyebadilika kabisa sura yake, alifanyiwa upasuaji huo kwa kutumia dola 250,000/- ambazo ni sawa na shilingi milioni 537.5.

Alves anayefanya kazi kwenye shirika moja la ndege, alizaliwa Brazil ingawa kwa sasa anaishi jijini London. Hivi karibuni alifanyiwa upasuaji mwingine ili kuweza kurekebisha tabasamu lake lionekane kubwa kidogo na hata macho yake yaonekane vizuri zaidi. Kijana huyo alisema kuwa kazi ya kujihusisha na upasuaji huo ni ndefu na unapoanza huwezi kuacha na inahitaji matunzo sana.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW