Michezo

Brazil waanza vyema kombe la dunia kwa kuichapa Croatia 3-1

Wenyeji wa michuano ya kombe la dunia, Brazil wameianza vyema baada ya kuichapa Croatia mabao 3-1.

1402608445846_lc_galleryImage_epa04252523_Thiago_Silva_
Croatia ndio walikuwa wa kwanza kupata bao baada ya mchezaji wa Brazil Marcelo kujifunga katika dakika 11. Brazil walijipatia goli lao la kuwasazisha kutoka kwa Neymar aliyezitikisa nyavu za Croatia katika dakika ya 29 kwa shuti la umbali wa yards 25. Mpaka timu hizo zinaenda mapumziko magoli yalikuwa 1-1.

article-2656584-1EB5BDBE00000578-805_634x500

Katika dakika ya 70 referee wa mchezo huo Yuichi Nishimura aliwapa penalty Brazil iliyotumiwa vyema na Neymar aliyeipa Brazil bao la pili.

Wakati zikiwa zimesalia dakika 2 kumalizika kwa mchezo huo, Brazil waliongeza bao la tatu lililofungwa kirahisi na Oscar aliyemwacha mlinda mlango wa Pletikosa akijitupab kujaribu kuuokoa bila mafanikio.

Ushindi wa Brazil umepokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki wengi waliokuwa wamefurika kwenye uwanja uliopo mjini Sao Paulo.

Michuano hiyo inaendelea tena Ijumaa hii kwa mechi ya Mexico vs Cameron, Spain vs Netherlands na Chile vs Australia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents