Habari

Breaking: Diddy apata ajali ya gari

TMZ imepata picha ya Diddy baada ya ajali hiyo na inasemekana alikuwa anatetemeka vibaya sana hivyo kumlazimu kukaa kwenye majani

Diddy amehusika kwenye ajali ‘serious’ ya gari huko Los Angeles, kwa mujibu wa TMZ.

Habari zinadai kuwa kuna gari ambayo iliigonga upande wa kushoto gari ya Diddy ambaye alikuwa akiendeshwa na dereva wa gari lake kugonga gari jingine.

Gari ya Diddy baada ya ajali

Maofisa waliitwa kwenye eneo la tukio na kudai kuwa kila mmoja aliyekuwa kwenye magari hayo alilalamika kuwa na maumivu akiwemo Diddy, dereva wake na dereva wa gari jingine.

Bado haijulikani ni kiasi gani wameumia lakini polisi wameiambia TMZ kuwa hakuna aliyepelekwa hospitali licha ya ambulance kuitwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents