Habari

BREAKING: Kundi la kigaidi la Al-Shabaab lakiri kutekeleza shambulizi la kigaidi la Westlands, Kenya

Msemaji wa kundi la kigaidi la Al-Shabab amekiri wazi kuwa, milipuko na milio ya risasi iliyotokea katika Hoteli ya Dusit mapema mchana wa leo huko Westlands jijini Nairobi nchini Kenya, limetekelezwa na kundi hilo.

Msemaji huyo ameliambia Shirika la Habari la BBC kwa njia ya simu, kuwa kundi hilo ndio lililotekeleza shambulizi hilo.

Hata hivyo, Msemaji huyo hajatoa maelezo zaidi, lakini amesema kundi hilo litatoa maelezo zaidi punde operesheni yao ikikamilika.

Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote rasmi ya vifo kwenye shambulizi hilo la kigaidi .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents