Diamond Platnumz

Breaking: Mama yake Diamond azidiwa, mwenyewe asema “mama yangu anaumwa sana”

Usiku huu Diamond kupitia website yake ameweka picha za mama yake ambaye ni mgonjwa aliyempeleka Marie Stopes baada ya kuzidiwa. Katika picha hizo Diamond akiwa na mtu aitwaye Dallas anaonekana mtu mwenye majonzi na wakati mwingine akilia kuashiria kuwa kweli mama yake amezidiwa.

Katika picha hizo pia mama yake anaonekana akitapika. Awali Diamond alikuwa ameweka maelezo kusimulia mkasa mzima lakini baadaye ameyatoa na kubakiza picha pekee yake. Bongo5 inamtakia mama yake Diamond afueni ya haraka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents