Uncategorized

BREAKING: Mgombea wa upinzani, Felix Tshisekedi ashinda uchaguzi DRC

Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi wa urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, tume ya uchaguzi imesema.

Matokeo ya awali yanaonyesha mgombea huyo wa upinzani amemshinda mgombea mwingine wa upinzani Martin Fayulu, pamoja na mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na serikali Emmanuel Shadary.

Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Ceni) Corneille Nangaa, alisema mapema Alhamisi kwamba Bw Tshisekedi alipata asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa na “anatangazwa mshindi wa urais mteule.”

Tshisekedi alipata zaidi ya kura 7 milioni naye bw Fayulu akapata kura takriban 6.4 milioni, huku mgombea wa serikali Emmanuel Ramazani Shadary akipata takriban kura 4.4 milioni.

Iwapo matokeo hayo yatathibitishwa, Bw Tshisekedi atakuwa mgombea wa kwanza kabisa wa upinzani kushinda uchaguzi wa urais tangu DRC ilipojipatia uhuru.

Bw Tshisekedi yuko kwenye muungano wa kisiasa aliyekuwa mgombea wa chama cha UNC (Union for the Congolese Nation) Vital Kamerhe UNC ambapo walikuwa wamekubaliana kwamba Tshiskedi atagombea wadhifa wa rais naye Kamerhe awe waziri mkuu iwapo muungano wao utashinda urais.

Wafuasi wa Felix Tshisekedi awali walikusanyika nje ya makao makuu ya chama chake Limete, Kinshasa Jumatano
Image captionWafuasi wa Felix Tshisekedi awali walikusanyika nje ya makao makuu ya chama chake Limete, Kinshasa Jumatano

Rais Joseph Kabila anatarajiwa kuondoka madarakani baada ya kuongoza kwa miaka 18.

Mgombea wake aliyemteua kuwakilisha muungano tawala Emmanuel Ramazani Shadary amemaliza wa tatu.

Martin Fayulu ambaye awali alikuwa mgombea wa pamoja wa muungano wa upinzani kabla ya Tshisekedi na mgombea wa chama cha UNC (Union for the Congolese Nation) Vital Kamerhe kujiondoa kutoka kwenye muungano huo na kuunda muungano wao wawili, alimaliza akiwa nafasi ya pili.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, CENI, matokeo kamili yanatarajiwa kutangazwa mnamo 15 Januari na rais mpya ataapishwa siku tatu baadaye. Matokeo hayo hata hivyo yanaweza kupingwa katika Mahakama ya Kikatiba.

Bw Kabila alikuwa ameahidi kukabidhi madaraka kwa mshindi wa uchaguzi huo, jambo ambalo likitokea itakuwa mara ya kwanza tangu DRC kupata uhuru kutoka kwa Ubelgiji mwaka 196

Matokeo hayo yalikuwa awali yametarajiwa kutangazwa Jumapili lakini yakaahirishwa.

Presentational grey line

Ushindi wa kihistoria

Mwandishi wa BBC Louise Dewast anasema ushindi huo uliotangazwa na CENI ni wa kihistoria kwa chama cha UDPS na Tshisekedi mwenyewe.

Chama hicho cha upinzani kimejaribu kwa miaka mingi kushinda uchaguzi DRC bila mafanikio. Lakini katika siku za karibuni kumekuwa na tetesi kuhusu uwezekano wa kufanyika kwa mwafaka kati ya Tshisekedi na rais Joseph Kabila hatua ambayo ilizua wasiwasi miongoni mwa wanasiasa wa upinzani.

Bw Tshisekedi mwenyewe amekiri kwamba alifanya mazungumzo na chama tawala lakini kuhusu maandalizi ya kipindi cha mpito.

Swali kuu kwa sasa ni jinsi wananchi na wadau wa kisiasa watayapokea matangazo hayo. Kanisa Katoliki ambalo lina waumini wengi na lilikuwa na waangalizi wa uchaguzi maeneo mengi lilikuwa limetahadharisha kwamba litayakataa matokeo iwapo hayatakuwa ya kweli. Kanisa hilo lilikuwa limesema linamfahamu mshindi wa urais na kwamba alikuwa ni mshindi wa wazi.

Presentational grey line

Felix Tshisekedi ni nani?

Felix Tshisekedi, ni mwanawe mwanzilishi wa chama cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS), mwanasiasa wa upinzani wa muda mrefu Etienne Tshisekedi.

Felix Tshisekedi akiwa katika mkutano wa kisiasa April 24, 2018
Image captionFelix Tshisekedi akiwa katika mkutano wa kisiasa Aprili 2018 mjini Kinshasa

Babake alifariki Februari mwaka jana na sasa mwanawe anatarajia kutumia msingi wa umaarufu wa babake kuchaguliwa kuwa rais.

Marafiki zake humuita kwa jina la utani “Fatshi” kutokana na hali kwamba yeye ni mnene kiasi.

Kwa muda ilionekana kana kwamba Tshishekedi, 55, jina lake halingekuwa kwenye karatasi za kura.

Novemba 11, yeye na Vital Kamerhe pamoja na wagombea wengine watano wa vyama vya upinzani walikutana na kumchagua Martin Fayulu apambane na Emmanuel Ramazani Shadary.

Lakini makubaliano yao yalidumu saa 24 pekee.

Tshisekedi na Kamerhe walidai kushinikizwa na vyama vyao kujiondoa na wakajitenga na Fayulu hatua iliyougawanya upinzani.

Wakishinda, Tshisekedi atakuwa rais naye Kamerhe, ambaye ni rais wa zamani wa Bunge na ambaye aliwania dhidi ya Kabila mwaka 2011 awe waziri mkuu.

Tangu babake Tshisekedi alipoanzisha chama cha UDPS mwaka 1982, kilihudumu kama chama kikuu cha upinzani, mwanzoni wakati wa utawala wa Mobutu Sese Seko kisha wakati wa utawala wa babake Kabila, Laurent-Desire Kabila, aliyeongoza 1997 hadi kifo chake 2001.JM

Kujiondoa kwa Tshisekedi kutoka kumuunga mkono Fayulu kulizua lalama, kwani kuliugawanya upinzani uliokuwa umeonesha dalili za kuungana.

Tshisekedi ni baba wa watoto watatu na yeye na Fayulu ni waumini katika kanisa moja la kipentekoste jijini Kinshasa.

Waliwania wanawania dhidi ya Shadary ambaye ni Mkatoliki.

Jean-Pierre Bemba December 23
Image captionJean-Pierre Bemba alizuiwa kuwania urais na tume ya uchaguzi lakini alikuwa anamuunga mkono Tshisekedi

Tshisekedi ana stashahada katika mauzo na mawasiliano kutoka Ubelgiji, lakini wakosoaji wake hutilia shaka hilo.

Wakosoaji wake pia wamekuwa wakisema hajawahi kushikilia wadhifa wowote wa juu au kuwa na uzoefu wa usimamizi.M

Lakini amepanda cheo chamani, kuanzia mwaka 2008 ambapo alikuwa katibu wa taifa aliyeangazia masuala ya uhusiano wa nje.

Machi mwaka jana aliteuliwa kiongozi wa chama baada ya kifo cha babake.

Alichaguliwa kuwa mbunge 2011, akiwakilisha eneo la Mbuji-Mayi katika mkoa wa Kasai-Oriental lakini alikataa kuhudumu kwa kuwa hakutambua kushindwa kwa babake na Rais Kabila katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2011.

Tshisekedi, ingawa hana uungwaji mkono mkubwa kama wa babake, aliambia AFP mwaka jana kwamba akishinda urais ataunda tume ya ukweli, haki na maridhiano na kumuwajibisha Bw Kabila. Lakini alisema atamruhusu kusalia nchini DR Congo.

Katumbi
Image captionMoise Katumbi alizuiwa kurejea nchini DRC

Walioruhusiwa kuwania urais DR Congo

  • Emmanuel Ramazani Shadary
  • Kikuni Masudi Seth
  • Mukona Kumbe Kumbe Pierre
  • Ngoy Ilunga Isidore
  • Makuta Joseph
  • Kabamba Noel
  • Mabaya
  • Kinkiey Mulumba
  • Freddy Matungulu
  • Felix Tshisekedi
  • Allain Shekomba
  • Radjabu Sombolabo
  • Kamerhe Vital
  • Fayulu Martin
  • Bomba
  • Gabriel Mokia
  • Basheke Sylvain
  • Charles Gamena
  • Mbemba Francis
Presentational grey line

Wagombea urais wakuu

Composite of three candidates (L-R): Martin Fayulu, Emmanuel Shadary and Felix Tshisekedi
Image captionWagombea wa upinzani Martin Fayulu (Kushoto) na Felix Tshisekedi (Kulia) wanashindana na waziri wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Shadary (Kati)

Kulikuwa na wagombea 21 lakini watatu ndio wakuu:

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents