PichaUmbea

Model Jack Patrick Afikishwa Mahakamani!

Model wa Kitanzania, ambaye utamtambua kama Video chick wa baadhi ya nyimbo za Bongo flava zilizohit kama ‘Nataka Kulewa’ ya Diamond na ‘She got a gwan’ ya Ngwair, Jacqueline Patrick aka Boss Lady, amefikishwa mahakamani kwa kosa la kumpiga na chupa na kumjeruhi msichana aliyetambulika kwa jina la ‘Hafsa Sasya’. I know, Shocking right??

Story yenyewe inasemekana kuenda hivi:

Jack Patrick akiwa mahakamani
Jack Patrick akiwa mahakamani
(Photo Credits: Simon da don)
Jumamosi ya Tarehe 26th January 2013, Jacque alikua akiparty katika kiwanja cha Elements iliyopo maeneo ya Masaki, Dar es salaam. Hafsa naye alikua kwenye same kiwanja akiwa amesimama na mshikaji wake. Then, Jack akawa anaenda msalani ambapo ndipo alimpiga kumbo Hafsa. Demu akashangaa, kwani vipi, ila akafanya kukausha. Hafsa anadai Jack alivyokua anarudi kutoka chooni, akampiga tena kumbo. Ndipo hafsa akamuondolea uvivu na kumuuliza Jack niaje!

Inasemekana Jack ndio akamwakia na ugomvi ukaanza na kuishia kwa Jack kumpiga Hafsa chupa na kumuumiza kiasi cha kushonwa nyuzi tatu.

trickj
(Photo Credits: Simon Da Don)
Hafsa alitoka ukumbuni hapo na kunyookea Obay polisi ambapo alifungua mashitaka na kusababishia Jack aitwe kufanyiwa mahjiano polisi.

Inasemekana Jack, amekiri kuwepo kwa kesi hiyo, bila kuongezea kingine chochote.

Baada ya kesi hiyo kusikilizwa Jumatano, imeahirishwa mpaka tarehe 3 ya March.

Jack Patrick aka Diva Boss Lady hivi karibuni amemake headlines zetu kwa Utajiri anauonyesha wa nyumba nzuri na Pimped out mdinga wa Mercedes Benz, pamoja na uhusiano wake mpya wa kimapenzi na Juma Jux, mbaya wa Chorus za Bongo Flava.

Tutaendelea kuwapa updates za story hii.

hafsa sasya akiwa ameumia

Hafsa Sasya akiwa ameumia
(Photo Credit: Jamii Forums)

Jack Patrick New Car
Jack Patrick New Car

Screen shot 2013-02-22 at 4.51.41 PM

jux

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents