Uncategorized

BREAKING NEWS: Idadi ya watu isiyojulikana wafukiwa na kifusi kwenye machimbo ya moram jijini Arusha

Idadi ya watu isiyojulikana wamefukiwa na kifusi kwenye machimbo ya moram yaliyopo eneo la Moshono mkoani Arusha. Juhudi za uokoaji bado zinaendelea.

Akizungumza na ITV Kamanda wa Polisi Jijini Arusha Jonathan Shana amesema kwamba juhudi za kuokoa waliofukiwa zinaendelea ambapo wamefanikiwa kuokoa watu wawili na kukimbizwa kwenye hospitali ya
Mount Meru kwa matibabu.

Kamanda Shana amesema kwamba kwa sasa kwenye shughuli za kuokoa waliyofukiwa tayari wamepata tingatinga lenye kijiko ambalo linafanya kazi hiyo.

Lakini awali vijana mkoani humo walijitokeza kwa wingi na kuanza kuchimba mchanga kwa kutumia sururu na kuwapongeza kwa ushirikiano waliyouonyesha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents