Tupo Nawe

Breaking news: Mo Dewji ajiuzulu uenyekiti wa Bodi Simba baada ya kipigo cha Mtibwa Sugar

Baada ya kupoteza fainali ya MapinduziCup Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya SimbaSC, Mohammed Dewji ametangaza kujiuzulu nafasi yake na kubaki kama Mwekezaji.

Mo ameandika ujumbe huo dakika chache tu baada ya Simba SC kupokea kichapo cha bao 1 – 0 kutoka kwa Mtibwa Sugar na kupelekea kukosa Ubingwa wa michuano ya kombe la Mapinduzi

Vijana wa Mtibwa Sukari walipata bao la mapema kunako dakika ya 38, kupitia kwa Awadhi Salum Juma ambalo limepelekea kudumu mpaka mwisho wa mchezo huo.

Simba SC na Mtibwa Sugar zote zilikuwa kundi B katika michuano hii group ambalo ndiyo limetoa be bingwa. Wakati Bingwa wa kombe la Mapinduzi 2010 Mtibwa Sugar wakiwasukumiza nje ya michuano hii Yanga SC kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya  dakika 90′ kumalizika  1-1 huku Simba SC  wakiwatoa Mabingwa watetezi Azam FC hatua ya nusu fainali

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW