BurudaniUncategorized

Breaking News: Muigizaji mkongwe Mzee Majuto afariki dunia

Msanii mkongwe wa vichekesho Amri Athuman’ King Majuto’ amefariki dunia usiku huu baada ya kulazwa siku chache zilizopita katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Mchekeshaji Joti ndio wa kwanza kutoa taarifa hizo kupitia mtandao wa instagram.

“R.I.P @Kingmajuto Umetuachia Maumivu Makubwa sana ktk Tasnia ya Comedy Tanzania Sisi wanao,Tutakukumbuka kwa kazi zako,Upendo wako,Tabasamu lako Daima milele,Tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi,Pumzika kwa Amani Mzee wetu,” aliandika Joti.

Mzee Majuto ambaye alijizolea umaarufu mkubwa kwenye filamu alianza kuugua mwaka jana na mwaka huu serikali kwa kushirikana na wananchi walichanga pesa na kumpelekeka kwenye matibabu nchini India.

Muigizaji huyo alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 9.

Related Articles

175 Comments

  1. Kila Mara tukio kama hili linapotokea hunichukua dakika 240 kujiuliza kuhusu maana kifo. Huwa ninasononeka kiasi cha kuona ninachofanya hapa duniani hakina maana yoyote. Lakini huishia kwa kujifariji tu kuwa “lipo tumaini kwa waaminio katika Mungu kuwa Babu yetu Mzee Majuto amepumzika tu, ipo siku ataungana na familia yake na watanzania wote, kazi tuliyonayo kwa sasa ni kusahihisha njia zetu, tudumu katika yale ambayo Mungu ametuagiza kuyafanya duniani. R.I.P KING MAJUTO

  2. Dah? tatzo la watanzania mtu akixhafkwa na umaut ndo mnapost na kumsfia kwa kla namna saiv kila mtu kapost kifo cha mzee majuto na kmpa kila sifa lakn kpnd yupo hai hakuna alyempost wala kumsifia tujiulze hii saport mnayoione kupost kifo mngekuwa mnaitoa kpnd anatoa kazi zake afadhal MUNGU MWENYE NGUVU AKUPOKEE MZEE MAJUTO.

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents