Habari

Breaking News: Boti ya kampuni ya Seagull imezama Zanzibar, abiria wanaendelea kuokolewa

Boti ya abiria MV Skagit kutoka kampuni ya Seagull imezama leo mchana katika eneo la Chumbe Mnara karibu kabisa na bandari ya znz. Boti hiyo ilikuwa ikitokea bandari ya znz kuja Dsm katika safari zake za kawaida majira ya saa 6 na nusu mchana na kupata hitilafu iliyosababisha boti hiyo kushindwa kuendelea na safari na kuanza kuzama kwa mujibu wa mdau wa bongo5 Zakari Khamis ambaye alikuwa akimngoja ndugu yake katika bandari ya boti jijini Dsm alipigiwa simu na ndugu yake akimtaarifu ajali hiyo na kwamba kwa mujibu wa maelezo yake watu wote waliwahi kujiokoa na kuokolewa kwa msaada wa watu mbali mbali waliowahi kufika katika eneo la bahari ilipotokea ajali hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents