Tragedy
Breaking News: Patrick Mafisango wa Simba SC Afariki Dunia.
Mchezaji Patrick Mafisango,amefariki dunia alfajiri baada ya gari alilokua anaendesha kupata ajali.
Kwa taarifa tulizozipokea, mchezaji huyo nguli ambaye ni raia wa Rwanda mwenye asili ya Congo, alikua anakwepa baiskeli mitaa ya Chang’ombe jijini Dar es salaam na ndipo akaingia kwenye Mtaro na gari na kufariki papo hapo.
Bongo5 inafanya jitihada za kupata taarifa za msiba kutoka kwa familia ya ndugu Mafisango ambapo tutazidi kuwahabarisha.
Taarifa hizi zimekuja kama pigo kubwa kwa wadau wapenzi n mashabiki wa mpira na wa mchezaji huyo, na mchezo huo umepoteza mcheaji mahiri.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.