Burudani

Breaking: Papaa Msofe atuhumiwa kwa mauaji


Yule promoter na mfanyabiashara maarufu nchini ambaye jina lake hutajwa sana kwenye nyimbo za dance, Papaa Msofe anashikiliwa na polisi jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za mauaji.
Papaa Msofe ambaye jina halisi ni Marijan Abubakari amekamatwa na polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni kutokana na mauaji ya Onesphori Kituli, mkazi wa Magomeni Mapipa, jijini Dar es Salaam.
Taarifa hizo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela.
Alisema kabla ya kutokea mauaji hayo, Papaa Msofe na marehemu walikuwa wakigombea nyumba ambayo ilikuwa imewekwa rehani kwa shilingi milioni 30.
Hata hivyo kuna taarifa kuwa kuna mtu mwingine ambaye anahusishwa na tuhuma hizo za mauaji japo bado hajakamatwa.
Kamanda huyo aliliambia gazeti la Nipashe kuwa Papaa Msofe alimpa marehemu fedha hizo kwa makubaliano kwamba ikiwa atashindwa kuzilipa atachukua nyumba yake.
Kabla ya mauji hayo ilidaiwa kwamba, Papaa Msofe na mwenzake walikuwa wakimtishia maisha marehemu huyo.
Kamanda Kenyela alisema kutokana na kuwepo kwa mgogoro huo, marehemu alifungua kesi mahakamani na kwamba siku ya hukumu alikutwa amekufa mbele ya mlango wa nyumba yake ingawa hakuna mali yoyote iliyochukuliwa.
Kwa mujibu wa Kamanda Kenyela, mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote baada ya upepelezi kukamilika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents