Michezo

Breaking: Sakata la uchaguzi Yanga, kamati ya utendaji yaitisha ghafla mkutano mkuu wadharura

Kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga imeamua kuhitisha mkutano mkuu wa dharura utakao fanyika tarehe 24 ya mwezi huu wa 11.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram Yanga imetoa taarifa hiyo huku ikiwa zoezi la kuchukua fomu za kuwania nyadhifa mbalimbali ndani ya klabu hiyo zikiendelea.

Wakati uchaguzi mkuu wa Yanga ukitarajiwa kufanyika tarehe 13 ya mwezi Januari hapo mwakani kupitia kwa mwenyekiti wa baraza la wadhamini ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika hapo jana siku ya Jumapili ametanabaisha kuwa aliyekuwa mwenyekiti wao, Yusuf Manji bado anaendelea kushikilia kiti hiko kwa mujibu wa barua waliyoipokea kutoka kwake.

“Kwenye mkutano mkuu ule wa wanachama, ilipigwa kura nani wanamtaka Manji arudi, wajumbe wote 4500 walisema tunamtaka Manji arudi na sisi katika baraza la wadhamini tukasema Manji aandikiwe barua “, amesema Mkuchika.

George Mkuchika ameongeza “Tukamuandikia barua na mimi mwenyekiti wa baraza ndiye niliyetia saini, amejibu Manji kwa kifupi anasema, “Nimepokea maamuzi ya wanachama wa Yanga, lakini bahati mbaya kipindi nimepokea nipo kwenye matibabu, tarehe 15 Disemba madaktari wanasema nitakuwa nimekamilika, nitaanza kuhudhuria ofisini mara kwa mara kuanzia 15, Januari.”

Pia, Mkuchika amesema kuwa klabu hiyo sasa ina mwenyekiti wake ambaye ni Yusuf Manji na suala hilo liko kihalali kwakuwa ni maamuzi ya mkutano mkuu.

Maoni mengine ambayo baraza la wadhamini imekubaliana ni pamoja na kuiagiza kamati ya utendaji ya Yanga kukaa meza moja na TFF ili kujadili juu ya kujaza jina la Yussuph Manji katika majina ya wagombea pamoja na kusuala la kusimamia uchaguzi wa klabu hiyo, ikitaka uchaguzi usimamiwe na kamati ya uchaguzi ya klabu badala ya TFF.

https://www.instagram.com/p/BqFbfcZAWeJ/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents