Michezo

BREAKING: Simba SC watupwa nje michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Yaungana na vijana wa Kinondoni KMC

Klabu ya Simba kutoka Tanzania imetolewa kwenye michuano ya Klabu bingwa barani Afrika kwa kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya UD Songo ya nchini Msumbiji.

Mechi hiyo iliyochezwa leo Agosti 25, 2019 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, UD Songo ndiyo waliokuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Simba kupitia kwa nahodha wake Luis kunako dakika 14 ya mchezo.

Goli la kusawazisha la Simba SC, Limefungwa na Erasto Nyoni kwa njia ya mkwaju wa penati kunako dakika ya 86 ya mchezo.

Mchezo wa kwanza Simba SC walitoka Srae ya 0-0 dhidi ya UD Sonko, Hivyo kwa matokeo hayo UD Sonko wanasonga mbele kwa faida ya goli la ugenini.

Simba SC inakuwa ni timu ya pili kutoka Tanzania kutolewa kwenye michuano kimataifa ya CAF, Baada ya klabu ya KMC FC ya Kinondoni kutolewa Ijumaa hii kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents