Habari

Breaking: Taharuki yatanda Nairobi, Milipuko na milio ya risasi yatawala

Milipuko na milio ya risasi yasikika katika eneo la 14 Riverside, Nairobi kunakopatikana hoteli ya DusitD2. Milipuko miwili mikubwa ya risasi ilisikika na baadaye ufyatuaji wa risasi.

Watu kadha wamejeruhiwa na wanahudumiwa na maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu wakisaidia na watu wengine wa kujitolea.

Mmoja wa majeruhi amesafirishwa kupelekwa hospitalini.

Maafisa wa polisi wamefika eneo hilo, katika jumba hilo ambalo lina hoteli yakifahari na afisi za kampuni mbalimbali.

Baadhi ya watu waliokwama kwenye vyumba vya jumba hilo wamekuwa wakiandika ujumbe kwenye mitandao wa kijamii wakieleza kwamba wamekwama, au kujificha.

Mkuu wa polisi wa uchunguzi wa jinai Bw George Kinoti ni miongoni mwa maafisa wakuu wa polisi waliofika kuratibu operesheni ya kuokoa watu waliokwama ndani.


Magari kadha yanawaka moto katika maegesho ya jumba hilo.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents