Habari

Breaking: Watu wasiojulikana wafyatua risasi na kumteka mfanyakazi wa shirika la misaada nchini Kenya

Kundi la watu wasiojulikana waliojihami wamemteka mwanamke mfanyakazi wa shirika la misaada, raia wa Italia kutoka kusini mashariki mwa Kenya, Polisi inasema.

Wanaume hao wanaoarifiwa kujihami kwa bunduki, “wamefyetua risasi kiholela” kabla ya kumteka msaidizi huyo mwenye umri wa miaka 23 kutoka mji wa pwani Malindi.

Watu watano pia wanaarifiwa kujeruhiwa na wamepelekwa hospitalini, mmoja kati yao akiwa yuko katika hali mahututi.

Haijajulikana wazi ni kwanini shambulio hilo limetokea na waliolitekeleza ni akina nani, polisi wanasema.

Hatahivyo, polisi imeeleza kwamba wanalichukulia tukio hilo, lililotokea mwendo wa saa mbili Jumanne usiku kama la kigaidi.

Katika ujumbe kwenye Twitter, idara ya Polisi nchini imesema wanaume hao walikuwa wamebebea bunduki aina ya AK47 walizozitumia kulivamia jumba la kibiashara la Chakama katika kaunti ya Kilifi pwani ya Kenya nje kidogo ya mji wa Malindi.

Polisi kwa sasa wametawanywa kuwasaka wahalifu hao.

https://twitter.com/KTNKenya/status/1065125061840068608

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents