Habari

BREXIT: Makubaliano mapya ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya ni ‘kaa la moto’

Uingereza na Umoja wa Ulaya wameafikiana makubaliano mapya ya Brexit, Yatakayofungua njia kwa nchi hiyo kujitoa rasmi katika Umoja huo mwezi October 31 mwaka huu.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson anatarajiwa kutoa taarifa kuhusu makubaliano hayo mapya ya mpango wa nchi yake kujitoa Umoja wa Ulaya  kwenye bunge la Uingereza kesho Jumamosi Oktoba 19, 2019.

Naye kiongozi wa Bunge la Uingereza, Jacob Rees- Mogg amesema wabunge watajadili iwapo wapitishe mpango mpya wa BREXIT au nchi hiyo ijitoe kwenye umoja huo bila makubaliano.

Waziri mkuu Boris Johnson aliyedhamiria kwa kila hali kuhakikisha nchi hiyo inaachana na Umoja wa Ulaya, Amesema amefikia makubaliano mapya yanayoipatia nchi yake udhibiti kamili.

Naye kiongozi wa mazungumzo hayo upande wa Umoja wa Ulaya, Michel Barnier, ameyapongeza makubaliano hayo akisema yanalinda maslahi ya Ulaya lakini pia ametahadharisha kuwa makubaliano hayo yanapaswa kupitishwa na Bunge la Uingereza ambalo limeshayakataa makubaliano ya Brexit mara tatu.

Hata hivyo, makubaliano hayo yanaweza tena kupingwa yatakapowasilishwa mbele ya Wabunge ili kuidhinishwa hiyo kesho Jumamosi.

Tayari Sarafu ya Uingereza ‘Pound’ imeshuka thamani katika masoko ya hisa kutokana na wasi wasi kama Bunge litayaidhinisha makubaliano hayo.

Imeelezwa kuwa imepoteza asilimia 0.34 ikilinganishwa na Dola ya Marekani, Wakatai huo huo sarafu ya Euro imepanda thamani kwa asili mia 0.69.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents